Kwa muda sasa wasomaji wa Tanzania Tech wamekuwa wakiuliza mbona kama Tanzania Tech imebadilishwa kutoka Kiswahili na kuwa Kingereza..?
Majibu ya swali hilo ni kuwa Tanzania Tech sasa inapatikana kwa lugha ya kiswahili na kingereza. Kupitia Tanzania Tech English utaweza kusoma habari mbalimbali na makala za teknolojia kwa kiingereza na kupitia Tanzania Tech utaendelea kufurahia makala mbalimbali kwa ajili ya watanzania, ikiwa pamoja na Maujanja pamoja na habari nyingine za teknolojia.
Tanzania Tech haijabadilika bali tumeongeza uwanja mpana zaidi wa wasomaji wetu ili kuweza kufikia watu wengi zaidi hata wanaotumia lugha ya Kiingereza.
Unaweza kupitia Tanzania Tech Kiswahili Hapa, na kama unataka kusoma makala za kiingereza unaweza kusoma Tanzania Tech English Hapa.